Mlipuko wa virusi vya corona 2019-20

Mlipuko wa Virusi vya Korona (kwa Kiingereza: Coronavirus) ulibainika rasmi tarehe za katikati za mwezi Desemba mwaka 2019 katika mji wa Wuhan huko China ya kati. Kulikuwa na kikundi cha watu wenye nimonia bila chanzo kinachoeleweka. Ulibainika baadaye kama aina mpya ya virusi vya korona. Tarehe 20 Januari 2020, Waziri Mkuu wa Uchina Li Keqiang, alitoa wito wa kutia juhudi katika kukomesha na kudhibiti janga la nimonia lililosababishwa na virusi vya korona. Kufikia tarehe 23 Machi, 2020, kesi 337,000 zimethibitishwa, Kufikia tarehe 5 Februari 2020, vifo 493 vilitokana na virusi hivyo tangu kifo cha kwanza kilichothibitishwa Januari 9, na watu 990 waliopona. Kifo cha kwanza nje ya Uchina kiliripotiwa tarehe 1 Februari nchini Ufilipino, kilikuwa ni kifo cha mwanamume wa Kichina mwenye umri wa miaka 44. Kumekuwa na majaribio ambayo yameonyesha kesi zaidi ya 6000 zilizothibitishwa nchini Uchina, ambazo baadhi zao ni za wafanyakazi wa huduma ya afya. Katikati ya Februari 2020 maswali mengi kuhusu virusi hivi vilibaki bila jibu, lakini Shirika la Afya Duniani lilitoa tathmini kuwa zaidi ya asilimia 80 za wagonjwa huonekana kuwa na ugonjwa mwepesi, wanapona kati ya asilimia za wagonjwa kuna maambukizi mazito yanayosababisha matatizo ya kupumua, hata nimonia, na asilimia 15 kudai walazwe hospitalini takriban asilimia 5 huwa na magonjwa hatari mnamo asilimia 2 hufa; hatari ya kifo inapatikana hasa kwa wazee, kuna mfano michache ya watoto. Baadaye imeonekana kwamba kiwango cha vifo si kubwa vile, labda kati ya % 0.5 hadi 1 lakini si rahisi kutaja kiwango kwa uhakika kwa sababu wengi walioambukizwa hawajulikani. utafiti wa ziada bado unahitajika kuna dalili kwamba virusi vya Covid-19 vinaweza kudumu hadi siku 8 kwenye uso wa kitu kilichoguswa na mgonjwa na bado kusababisha maambukizi Kufikia tarehe 11 Julai 2020, zaidi ya watu milioni 12.5 walithibitishwa kupatwa na COVID‑19 katika nchi na maeneo 188 duniani kote. Kati yao waliofariki ni zaidi ya 560,000 na waliopona ni zaidi ya milioni 6.89. Kufikia tarehe 15 Aprili 2022, WHO ilitangaza kuwa walitohibitishwa kuambukizwa ni 500.186.525, na kati yao 6.190.349 wamefariki, Marekani ikiwa nchi iliyoathiriwa zaidi (79.71 milioni walioambukizwa na 979.321 waliofariki, karibu 16% ya jumla ya dunia nzima), ikifuatwa na India (zaidi ya maambukizi milioni 43, na vifo 521.737) na Brazil (zaidi ya maambukizi milioni 30, na vifo 661.493).


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search